Home Kimataifa Mudavadi: Kenya inaunga mkono pendekezo la kusitisha vita Gaza

Mudavadi: Kenya inaunga mkono pendekezo la kusitisha vita Gaza

0
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi amesema Kenya inaunga mkono pendekezo la kumaliza vita kati ya  Israel na Hamas.

Mudavadi amesema kenya inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Misri, Qatar na Marekani kuhusu vita kati ya Israel na Hamas.

Taarifa hiyo, alisema inaangazia utaratibu wa kumaliza vita hivyo, uliotolewa na Rais Joe Biden wa Marekani ulio sambamba na wadau wanaojihusisha na juhudi za mashauriano ya kumaliza vita hivyo.

Mudavadi alisema kenya inaamini mapendekezo hayo yanapasa kuwa hatua ya mwanzo ya masharti ya Uhuru wa Wapalestina na kupatikana kwa amani kati ya pande hizo mbili.

Mudavadi alisema utekelezaji wa mapendekezo hayo utawapa afueni wapalestina  ambao kwa wakati huu wanakumbwa na mzozo wa kibinadamu,baa la njaa na vifo.

Alisema Kenya inakariri msimamo wake kwamba njia ya pekee ya kumaliza mzozo kati ya pande hizo mbili ni kuheshimu uhuru wao.

Mudavadi alizihimiza pande hizo mbili kukubali mapendekezo hayo ili kusaidia kuleta suluhu la kudumu.

Website | + posts