Home Habari Kuu Mudavadi: Kenya iko tayari kumlaki mfalme na malkia

Mudavadi: Kenya iko tayari kumlaki mfalme na malkia

0

Waziri aliye na mamlaka makuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi amesema Kenya iko tayari kabisa kwa ziara ya mfalme Charles wa Tatu na mkewe Malkia Camila.

Mudavadi alikutana na Balozi wa Uingereza humu nchini Neil Wigan OBE, ambaye alifahamisha kuhusu maandalizi ya ziara ya kiongozi huyo humu nchini.

Bwana Wigan alifahamisha Mudavadi kuhusu hatua ambazo wamepiga kwenye maandalizi akisema ni ya kufana.

Mudavadi kwa upande wake alimhakikishia Wigan kuhusu kujitolea kwa serikali kuhakikisha ziara ya mfalme Charles na Malkia Camila inafanikiwa.

“Taifa letu liko ange kumkaribisha mfalme Charles III na Malkia Camila. Ziara hii inaashiria uhusiano mwema na WA muda mrefu kati ya nchi hizi mbili na pia inatoa fursa ya kuuboresha hata zaidi kupitia kutambua sekta za ushirikiano kwa faida ya Mataifa haya mawili.

Mfalme Charles wa Tatu na mkewe Malkia Camila watazuru Kenya Oktoba 30 hadi Novemba 3, 2023.