Home Habari Kuu Mudavadi: Hatua ya Kenya kuondoa hitaji la viza itaimarisha uchumi

Mudavadi: Hatua ya Kenya kuondoa hitaji la viza itaimarisha uchumi

Mudavadi alipongeza agizo hilo, akisema litaimarisha pakubwa uchumi wa taifa hili.

0

Waziri mwenye mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, amesema hatua ya serikali ya kuondoa hitaji la viza kwa raia wa kigeni wanaozuru hapa nchini, itapiga jeki sekta ya utalii na kuvutia uwekezaji zaidi hapa nchini 

Waziri huyo wa mambo ya nje alisema kuwa wizara kadhaa, na idara za serikali zitahakikisha ufanisi katika utekelezwaji wa agizo hilo, litakaloanza mwezi Januari mwaka 2024.

“Mnamo mwezi Januari mwaka  2024, Kenya itafungua milango yake Kwa watalii, wawekezaji na wale wanaotaka kujifunza kuhusu demokrasia,uongozi bora na utangamano wa kijamii,” alisema Mudavadi.

Mudavadi alipongeza agizo hilo, akisema litaimarisha pakubwa uchumi wa taifa hili.

Akitangaza hatua hiyo jana Jumanne wakati wa sherehe ya Jamhuri, Rais William Ruto alisema agizo hilo litachochea ukuaji wa uchumi na kijamii wa taifa hili.

Ili kutekeleza sera hiyo mpya, Rais Ruto alisema a serikali imebuni mfumo wa kidijitali wa kuwatambua wageni wote wanaoingia hapa nchini.

Website | + posts