Home Habari Kuu Mudavadi atua Ghana kuhudhuria Mkutano wa Ulipaji Fidia wa Afrika

Mudavadi atua Ghana kuhudhuria Mkutano wa Ulipaji Fidia wa Afrika

0

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi amewasili nchini Ghana ambako amepangiwa kuhudhuria Mkutano wa Ulipaji Fidia wa Afrika.

Mkutano huo utaandaliwa leo Jumanne jijini Accra.

Punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kotoka, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje alilakiwa na maafisa waandamizi wa serikali ya Ghana.

Mkutano huo wa siku nne utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dunia, na unalenga kuangazia madhila ya kihistoria iliyokumbana nalo bara la Afrika wakati wa ukoloni, ukoloni mambo leo, ubaguzi na ubaguzi wa rangi.

Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kukuza Msimamo wa Pamoja katika Kupigania Haki na Malipo ya Fidia kwa Waafrika”.

Website | + posts