Home Taifa Mudavadi atoa wito wa umoja wa Afrika kuibadilisha UNSC

Mudavadi atoa wito wa umoja wa Afrika kuibadilisha UNSC

0

Kenya imetoa wito wa bara la Afrika kuwa na msimamo mmoja katika kushinikiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, UNSC kufanyiwa mabadiliko.

Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Musalia Mudavadi amesema Afrika ni sharti itumie fursa iliyopo sasa kutafuta uungwaji mkono wa kisiasa kwa ajili ya Baraza la Usalama kufanyiwa mabadiliko ya haraka yanayotoa kipau mbele kwa uwakilishi wa bara hilo katika baraza hilo.

Aliongeza kuwa mchakato wa kulifanyia baraza hilo mabadiliko lazima utambue kuwa Afrika inapaswa kushughulikiwa kwa njia ya kipekee na inayopaswa kupewa kipau mbele.

“Kutowakilishwa kwa Afrika katika kategoria ya kudumu na uwakilishi wa chini katika kategoria isiyokuwa ya kudumu, katika taasisi ya Umoja wa Mataifa ambayo imekabidhiwa jukumu la msingi la kudumisha amani na usalama duniani, ni ukosefu wa usawa wa kihistoria unaohitaji kuangaziwa kwa dharura,” alisema Mudavadi

“Kama eneo, tunapaswa kuungana; tunapaswa kuwa tayari na tunapaswa kuwa wazi kuzingatia kivitendo na kimkakati mitazamo yote, alimradi haihatarishi misingi mikuu ya Msimamo wa Kawaifa wa Afrika (CAP)”.

Mudavadi aliyasema hayo wakati wa mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Kamati ya Kumi (C-10) ya Umoja wa Afrika juu ya marekebisho ya UNSC unaoendelea mjini Algiers, Algeria.

Aliongeza kuwa Mkutano wa 11 wa Ngazi ya Mawaziri umekuja wakati unaofaa na hasa ni muhimu kuelekea Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Siku Zijazo utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Kulingana naye, kwa kuzingatia uhalisia unaobadilika wa usalama wa dunia, na kushindwa mara kadhaa kwa Baraza la Usalama kuchukua hatua pale hatua ya dharura inapohitajika, ni shati Afrika kusimama na kuhesabika.

Martin Mwanje & OPCS
+ posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here