Home Habari Kuu Mudavadi atoa wito wa kufanikishwa kwa demokrasia, usawa na haki

Mudavadi atoa wito wa kufanikishwa kwa demokrasia, usawa na haki

Waziri huyo aliwahimiza wakenya kukumbatia maendeleo kwa ustawi wa taifa hili.

0

Waziri mwenye mamlaka makuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi, ametoa wito wa kufanikisha demokrasia, usawa na haki huku Kenya ikisherehekea miaka 60 ya uhuru.

Mudavadi alisema kupandishwa kwa bendera ya Kenya kuliashiria kutekelezwa kwa juhudi za pamoja za kujenga taifa hili, ambapo kila mwananchi anapata fursa ya kunawiri bila kuzingatia hali yake, iwapo anaishi hapa nchini Kenya au ughaibuni.

“Tunatoa changamoto kwa raia wa Kenya kuwekeza ughaibuni jinsi wanavyowekeza nchini Kenya. Tunaposherehekea siku kuu ya Jamuhuri, tunajitolea upya katika nguzo zinatotuongoza za demokrasia, usawa na haki,” alisema Mudavadi.

Akizungumza Jijini London nchini Uingereza, waziri huyo aliwahimiza wakenya kukumbatia maendeleo kwa ustawi wa taifa hili.

Aidha Mudavadi, alitabua ufanisi mkumbwa kutokana na ziara ya mfalme Charles na Malkia Camilla hapa nchini hivi majuzi.

Ziara hiyo iliyotokana na mwaliko wa Rais William Ruto, ilihusisha miji ya Nairobi, Mombasa na viunga vyake.

Website | + posts