Home Habari Kuu Mudavadi ashutumu mashambulizi yaliyotekelezwa Moscow

Mudavadi ashutumu mashambulizi yaliyotekelezwa Moscow

Waziri huyo mwenye mamlaka makuu alikariri msimamo wa Kenya katika kulaani vitendo vya kigaidi na itikadi kali kote duniani.

Waziri Mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi, amejiunga na viongozi wa dunia katika kulaani mashambulizi ya mauaji yaliyotekelezwa na watu waliojihami kwa bunduki ambapo waliwaua zaidi ya watu 90 na kuwaacha zaidi ya 140 wakiwa wamejeruhiwa jijini Moscow nchini Russia.

Kwenye taarifa iliyowasilisha kwa mwenzake wa Urusi Sergey Viktorovich Lavrov, Mudavadi, ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje,  alisema taifa hili linalaani vitendo huivyo vya kihuni na linajiunga na Urusi katika kuomboleza mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Aliwasilisha risala zake za rambi rambi kwa walioathiriwa na vitendo hivyo vya kinyama akisema vitendo vya kigaidi na itikadi kali havikubaliki na ni ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Waziri huyo mwenye mamlaka makuu alikariri msimamo wa Kenya katika kulaani vitendo vya kigaidi na itikadi kali kote duniani.

Website | + posts
Radio Taifa
+ posts