Home Habari Kuu Mudavadi akabidhiwa rasmi Wizara ya Mambo ya Nje

Mudavadi akabidhiwa rasmi Wizara ya Mambo ya Nje

Afisi ya Mudavadi iliongezewa majukumu katika mabadiliko yaliyofanyiwa Baraza la Mawaziri na Rais William Ruto mapema mwezi huu.

0

Musalia Mudavadi amekabidhiwa rasmi Wizara ya Mambo ya Nje.

Mudavadi ambaye pia ni Waziri mwenye Mamlaka Makuu alikabidhiwa wizara hiyo na mtangulizi wake Dkt. Alfred Mutua.

Dkt. Mutua kwa sasa ni Waziri wa Utalii kufuatia mabadiliko ya kwanza kuwahi kufanywa na Rais William Ruto kwa Baraza la Mawaziri.

Hafla ya kumkabidhi rasmi Mudavadi mikoba ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje iliandaliwa leo Jumanne katika afisi ya Mudavadi iliyoko katika eneo la Railways jijini Nairobi.

Mudavadi ameahidi kutetea maslahi ya Kenya katika ngazi za kimataifa kwa manufaa ya ustawi wa uchumi wa taifa hili.

Aidha, anasema ataimarisha  ushirikiano na mataifa mengine kupitia kwa mikataba na juhudi nyingine za kimataifa.

Kwa upande wake, Dkt. Mutua aliahidi kuunga mkono juhudi za serikali za kutekeleza ahadi ilizotoa kwa Wakenya wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

 

Website | + posts