Home Biashara Mudavadi aisihi Afrika kushughulikia kusuasua kwa sekta ya kahawa

Mudavadi aisihi Afrika kushughulikia kusuasua kwa sekta ya kahawa

0
kra

Kenya imetoa kipaumbele kwa kahawa kama moja ya sekta muhimu zinazopaswa kufanyiwa mabadiliko ya haraka ili kuhakikisha ustawi wa uchumi.

Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi anasema serikali imeunda mipango mbalimbali inayolenga kuongeza uzalishaji kahawa nchini kutoka tani 51,000 zilizozalishwa mwaka 2021/22 hadi tani 100,000 kufikia mwaka 2025.

kra

Mudavadi anasema hatua hii itachangia ongezeko la uzalishaji wa kahawa ya bara la Afrika duniani.

Aidha alisema uzalishaji wa kahawa nchini umekuwa ukipungua miaka iliyopita kutokana na changamoto kama vile mabadiliko ya tabia nchi, bei kuyumba mara kwa mara, upatikanaji wa soko na utumiaji mdogo wa kahawa nchini miongoni mwa zingine.

“Kupungua kwa uzalishaji kumeathiri pakubwa mapato ya wakulima na hali yao ya maisha. Kenya imetoa kipaumbele kwa mabadiliko ya haraka kwa sekta ya kahawa katika ajenda yetu ya maendeleo ya kiuchumi yanayojulikana kama Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi kutoka Watu wa Tabaka la Chini hadi wa Juu (BETA) kama ilivyoelezwa katika manifesto ya serikali ya Kenya Kwanza ya Mwaka 2022-2027,” alisema Mudavadi.

Aliyasema hayo nchini Uganda leo Jumanne wakati wa Mkutano wa pili wa Kahawa Afrika unaofanywa chini ya kaulimbiu ya “Ubadilishaji wa sekta ya kahawa ya Afrika kupitia uongezaji thamani.”