Home Habari Kuu Mudavadi ahudhuria kongamano la usimamizi wa bahari

Mudavadi ahudhuria kongamano la usimamizi wa bahari

0

Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje amehudhuria kongamano la sera la ngazi za juu lililoangazia usimamizi wa bahari na uchumi wa samawati. 

Kongamano hilo liliandaliwa pembezoni mwa Baraza Kuu la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika, AU jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Lilidhamiria kutafuta namna ya kuimarisha ushirikiano wa bahari wa Afrika na Uaya na kutumia rasilimali za bahari kuchochea maendeleo barani Afrika.

Kongamano hilo lilidhaminiwa kwa pamoja na mataifa ya Comoros, Ushelisheli, Ureno, Wakfu wa Afrika na Ulaya, Tume ya AU na Umoja wa Ulaya.

Mudavadi alihudhuria kongamano hilo akiwa ameandamana na Balozi wa Kenya nchini Ethiopia, George Orina.

Website | + posts