Home Taifa Mudavadi aelekea Japani kuhudhuria mkutano wa TICAD

Mudavadi aelekea Japani kuhudhuria mkutano wa TICAD

0
kra

Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi ameondoka nchini kuelekea Japani ambako amepangiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo (TICAD) wa ngazi ya mawaziri utakaoandaliwa jijini Tokyo. 

Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, UN, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, UNDP, Benki ya Dunia na Tume ya Umoja wa Afrika, AUC.

kra

Wakati wa mkutano huo, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje atazungumzia uhamasishaji wa biashara na uwekezaji na kusisitiza maslahi ya serikali ya Kenya kuambatana na utekelezaji wa mpango wa Ajenda ya Mabadiliko kuanzia Chini hadi Juu, BETA.

“Mudavadi atatumia fursa hiyo kutoa wito wa ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kutimizwa kwa malengo endelevu ya maendeleo, SDGs na mabadiliko ya mfumo wa ufadhili wa kimataifa,” amesema Jacob Ng’etich, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano katika afisi ya Mudavadi.

Pembezoni mwa mkutano huo, Mudavadi atafanya mikutano na Mawaziri wa Mambo ya Nje Yoko Kamikawa wa Japani na Sara Beysolow wa Liberia.

 

Website | + posts