Home Kaunti Mtahiniwa kufanyia mtihani hospitalini Narok Kusini

Mtahiniwa kufanyia mtihani hospitalini Narok Kusini

0

Mtahiniwa mmoja wa mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE katika kaunti ndogo ya Narok Kusini, atafanyia mtihani wake hospitalini baada ya kushikwa na uchungu wa kujifungua siku moja tu kabla ya mtihani kuanza.

Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Narok Apollo Apuko alitoa hakikisho kamba msichana huyo atapatiwa usaidizi unahitajika ili kuhakikisha anafanya mtihani bila matatizo.

Apuko aliyasema hayo asubuhi ya leo, wakati wa ufunguzi wa kasha la karatasi za mtihani katika afisi ya kamishna wa kauntu ya Narok shughuli iliyoshuhudiwa na kamati ya usalama ikiongozwa na kamishna wa kaunti Isaac Masinde.

Watahiniwa 14, 544 wanafanya mtihani wa kidato cha nne KCSE, 43,465 wanafanya mtihani wa darasa la nane KCPE huku wengine 39,976 wakifanya mtihani wa KPSEA.

Vituo vya mtihani wa kidato cha nne KCSE katika kaunti ya Narok ni 189, vya KCPE ni 831 na vya KPSEA ni 932.

Kamishna Masinde aliwataka wote ambao wanasimamia mitihani hiyokuhakikisha wanafanya kazi nzuri kulingana na kanuni za mtihani akisema kwamba wale ambao watakiuka viwango vya mitihani watachukuliwa hatua ipasavyo.
the standards of the exam will be dealt with accordingly.

Aliwataka wasimamizi wa vituo vya mitihani kuwa na uwazi, wasijaribu kuiba mtihani akisema kundi la maafisa wa idara mbali mbali kutoka kwa wizara za elimu, mambo ya ndani na mawasiliano wanatekeleza uangalizi ili kuhakikisha mtihani hauvujishwi.

‚ÄúTusijaribu kushawishi watoto wetu kuiba mtihani kwa sababu wamekuwa wakijiandaa kwa miaka mingi kwa mitihani hii.” alisema Kamishna Masinde huku akisisitiza kwamba wasimamizi wa vituo wanafaa kuwa macho kuhakikisha kwamba hakuna ukiukaji wa taratibu.

Wageni hawataruhusiwa kwenye vituo vya mitihani.

Katika eneo la Maasai Mau, ambapo watu walifurushwa hivi maajuzi kutoka kwenye ardhi ya msitu, watahiniwa wataruhusiwa kufanya mitihani yao.

Wafungwa 10 katika gereza la Narok GK wanafanya mitihani leo kulingana na msimamizi wa gereza Benson Lomeri.