Home Kimataifa Mtaalamu wa vilipuzi katika kundi la ADF akamatwa

Mtaalamu wa vilipuzi katika kundi la ADF akamatwa

0

Jeshi la Uganda kwa ushirikiano na lile la Congo,limefanikiwa kukamata mtaalamu wa vilipuzi wa kundi haramu la Allied Democratic Forces – ADF katika oparesheni inayoendelea kwa jina “Operation Shujaa”.

Anywari Al Iraq au ukipenda AA alikamatwa Jumamosi Mei, 18, 2024.

Mtaalamu huyo wa vili[uzi ni mzaliwa wa wilaya ya Busia, mashariki mwa Uganda na wakati wa kukamatwa, alipatikana na silaha mbali mbali kama bunduki, risasi 45, vifaa vitatu vya mawasiliano na vifaa vya kutengeneza vilipuzi.

Wakati huo huo watoto wanne na wanawake watano waliokolewa katika mkoa wa Ituri ulio katika eneo la mashariki la jamhuri ya Congo. Walipatiwa huduma za dharura za kimatibabu huku mipango ikiwekwa ya kuwahamishia hospitali bora kwa matibabu zaidi.

Majeshi ya nchi hizo mbili yanashirikiana katika oparesheni ya kufurusha waasi wa kundi la ADF.