Home Kimataifa Mswada wa Mawasiliano na Uhusiano mwema waibua wasiwasi bungeni

Mswada wa Mawasiliano na Uhusiano mwema waibua wasiwasi bungeni

Hayo yanajiri huku wabunge kadha wakielezea wasiwasi wao kuhusiana na utekelezaji wa mswada huo,  licha ya wao waliuidhinisha.

0
kra

Mswada kuhusu mawasiliano na Uhusiano Mwema, sasa unatathminiwa na kamati ya bunge kuhusu habari, mawasiliano na uvumbuzi.  

Hayo yanajiri huku wabunge kadha wakielezea wasiwasi wao kuhusiana na utekelezaji wa mswada huo,  licha ya wao waliuidhinisha.

kra

Wakiwasilisha maoni yao kuhusu mswada huo kwa kamati hiyo, waakilishi wa mashirika tofauti kikiwemo chama cha wataalam wa maswala ya uhusiano mwema pamoja na taasisi ya wahasibu nchini, walitumai kuwa maoni yao yatachangia pakubwa kuboresha mswada huo hasa kuhusu utoaji wa mafunzo na usajili wa wataalam katika sekta tofauti.

Akiongea wakati wa kikao hicho, mbunge  wa Dagoretti kusini John Kiarie alikariri umuhimu wa kuzinduliwa kwa mfumo muafaka wa kuwasajili wataalam hao kuambatana na mswada huo.

Kwa upande wake mwakilishi mwanamke kaunti ya Baringo Flowrence Jematiah,alielezea wasiwasi kuhusu uwezo wa Mswada huo wa kuepusha migogoro katika siku zijazo.

Alitaka kujua iwapo mswada huo utatatua swala la kufeli kwa mawasiliano hatua iliyosababisha maandamano yaliyoongozwa na vijana hapa nchini.

Mswada huo utaendelea kuchambuliwa hasa kuhusu jinsi utakavyoboresha sekta ya uhusiano mwema wa umma na mawasiliano nchini.

Mswada huo unatarajiwa kutoa mwelekeo kwa hali ya baadaye ya sekta hiyo na wajibu wake katika ustawi wa taifa hili.

Website | + posts