Home Kimataifa Upatikanaji wa cheti cha kuzaliwa na kifo: Mswada wasomwa bungeni

Upatikanaji wa cheti cha kuzaliwa na kifo: Mswada wasomwa bungeni

0
Martha Wangari - Mbunge wa Gilgil
kra

Mswada wa (Marekebisho) ya Usajili wa Kuzaliwa na Kifo 2014 umesomwa kwa mara ya kwanza katika Bunge la Taifa. 

Mswada huo umewasilishwa bungeni na mbunge wa Gilgil Martha Wangari.

kra

Unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za usajili wa kuzaliwa na kifo kote nchini kwa kuanzisha angalau ofisi moja ya usajili katika kila eneo bunge.

Kwa sasa, kuna ofisi kama hizo 143 pekee nchini na kufanya iwe vigumu kupata vyeti muhimu kama vile vya kuzaliwa na kifo.

Mswada huo umependekeza kifungu nambari 6(3) cha katiba kufanyiwa marekebisho. Kifungu hicho kinaelezea kuwa kila Mkenya ana haki ya kusajiliwa kama raia.

Kwa kuongeza idadi ya ofisi za usajili, serikali inakusudia kufanya iwe rahisi kwa raia kupata haki hii na huduma zingine zinazohitaji uthibitisho wa utambulisho.

Ikiwa utapitishwa, Wakenya hasa wale wanaoishi vijijini na jamii zilizotengwa, watapunguza muda na juhudi zinazotakikana kupata cheti cha kuzaliwa na kile cha kifo.

Vyeti hivyo ni muhimu kwa upatikanaji wa elimu, huduma za afya, ajira na huduma zingine za jamii.

 

Website | + posts