Mswada wa kumbandua mamlakani Naibu Rais Rigathi Gachagua umepita hatua ya kwanza bungeni Jumanne alasiri. Hii ni baada ya Spika wa bunge wa kitaifa Moses Wetang’ula kuuruhusu kuwasililishwa kwa kuafiki viwango vinavyohitajika.
Mwasilishi wa mswada huo mbunge wa Kibwezi Magharibi Eckomas Mwengi Mutuse.
Akiwasilisha mswada huo, Mutuse amesoma sababu za kutaka kumbandua Rigathi afisini zikiwemo matumizi mabaya ya afisi, ufisadi, kueneza chuki miongoni mwa Wakenya na kuwatishia maafisa wa umma.
Jumla ya wabunge 291 walisaini hoja hiyo ya kumtimua Rigathi huku 58 wakikosa kuisaini.
Kulingana na sheria, mswada huo utaanza kujadiliwa baada ya siku tatu baada ya kuwasilishwa leo.
Wabunge walionekana kuuunga hoja hiyo kwa wingi huku wakipiga kelele za shangwe na nderemo wakati Mutuse akiiwasilisha.