Home Taifa Mswada wa Fedha 2024 kuwasilishwa bungeni leo Jumanne

Mswada wa Fedha 2024 kuwasilishwa bungeni leo Jumanne

0
kra

Macho ya Wakenya yataelekea kwenye bunge la kitaifa ambako Mswada wa Fedha 2024 unatarajiwa kuwasilshwa leo Jumanne. 

Mswada huo umekumbana na pingamizi za kila aina kutoka kwa Wakenya wanaohofia kuwa utafanya gharama ya maisha ambayo tayari imewaelemea kupanda hata zaidi.

kra

Ili kudhihirisha kuwa mswada huo unakumbana na pingamizi kutoka kila pembe, baadhi ya wanaharakati wamefanga kufanya maandamano hadi kwenye majengo ya bunge leo Jumanne ili kuwashinikiza wabunge kuukatalia mbali.

Wabunge wa mrengo wa Azimio tayari wamesema kuwa wataupinga mswada huo utakapowasilishwa bungeni kwa kile wanachoelezea kuwa  kiwa utapitishwa jinsi ulivyo, utawakandamiza Wakenya.

Wabunge wa muungano unaotawala wa Kenya Kwanza leo Jumanne asubuhi walikutana katika Ikulu ya Nairobi na inatazamiwa kwamba wengi wao wataunga mkono mswada huo unaolenga kuongeza mapato yanayokusanywa na serikali ili kufadhili miradi mbalimbali.

Miongoni mwa masuala ambayo yamekumbana na pingamizi kali kwenye mswada huo ni pamoja na nia ya kutoza bidhaa kama vile mkate ushuru thamani wa ziada, VAT na pia kuwatoza ushuru wa asilimia 2.5 wamiliki wa magari nchini.

Haijabainika ikiwa baadhi ya mapendekezo hayo tata yameondolewa kwenye mswada huo na kamati ya fedha na mipango ya kitaifa inayoongozwa na mbunge wa Molo Kuria Kimani na ambayo ilisikiliza maoni ya Wakenya kuhusu mswada huo.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here