Home Kaunti Mshukiwa wa ulanguzi wa bangi anaswa Kisii

Mshukiwa wa ulanguzi wa bangi anaswa Kisii

Gari hilo na bangi iliyonaswa zilipelekwa katika kituo cha polisi cha Central mjini Kisii.

0
Mshukiwa wa ulanguzi wa bangi akamatwa Kisii.
kra

Maafisa wa polisi wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati, aliyekuwa akisafirisha kilo 146 za bangi katika barabara ya Kisii-Migori.

Kupitia mtandao wa X, idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI, ilisema kuwa baada ya maafisa wa polisi kupashwa habari, waliweka kizuizi cha barabarani katika eneo la Iyabe Bomokora.

kra

Gari aina ya Prado TX lenye nambari za usajili KDG 508E liliwasili, likiwa na watu wawili ndani. Walipoamriwa kusimama walitoroka huku maafisa hao wakiwaandama.

Kulingana na DCI, gari hilo liliingia kwa mtaro, huku dereva wake akitoroka. Maafisa hao walimkamata Collins Otieno na sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Suneka huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Gari hilo na bangi iliyonaswa zilipelekwa katika kituo cha polisi cha Central mjini Kisii.

Ndani ya gari hilo maafisa hao pia walipata nambari za usajili wa gari KDL 841X zikiwa kwenye mfuko.

Idara hiyo ilisema inamsaka mshukiwa aliyetoroka.

Website | + posts