Home Kimataifa Mshukiwa wa ugaidi Mohamed Abdi Ali kufahamu hatima yake Jumatatu

Mshukiwa wa ugaidi Mohamed Abdi Ali kufahamu hatima yake Jumatatu

Mahakama iliwaachilia huru Nuseibah Mohamed Haji, Alias Umm Fidaa na almaarufu Ummu Fidaa waliokuwa wameshtakiwa pamoja na mshukiwa huyo.

0
Mshukiwa wa ugaidi Mohamed Abdi Ali.
kra

Mshukiwa mmoja wa ugaidi aliyefunguliwa mashtaka ya kujaribu kubuni tawi la kundi la kigaidi ya Isis humu nchini na katika eneo la afrika mashariki mwaka 2016, atajua hatima yake leo Jumatatu.

Mahakama moja hapa Nairobi inatarajiwa kutangaza hukumu dhidi ya mshukiwa huyo Mohamed Abdi Ali almaarufu kama Abu Fidaa, na Abu Shuhadaa, ambaye tarehe 12 mwezi huu alipatikana na hatia ya kuwa mwanachama wa kundi hilo la kigaidi la ISIS.

kra

Ali aliyekuwa akihudumu kama daktari eneo la Wote kaunti ya Makueni, pia alipatikana na hatia ya kuandaa mkutano wa kuunga mkono makundi ya kigaidi na kuwasajili wanachama wapya wa makundi hayo.

Akitoa kauli yake,hakimu mkuu wa mahakama za milimani Martha Mutuku aliamua kuwa upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha dhidi ya Mohammed Abdi Ali kupitia mashahidi 26 wakiwemo maafisa wa kitengo cha kukabiliana na ugaidi cha ATPU, maafisa wa kitengo cha upelelezi cha Amerika cha FBI na maafisa wa polisi kutoka Uganda.

Hatahivyo mahakama iliwaachilia huru Nuseibah Mohamed Haji, Alias Umm Fidaa na almaarufu Ummu Fidaa waliokuwa wameshtakiwa pamoja na mshukiwa huyo.