Home Habari Kuu Mshukiwa wa mauaji ya Rahab Karisa kusalia kizuizini

Mshukiwa wa mauaji ya Rahab Karisa kusalia kizuizini

0

Mshukiwa mkuu katika mauaji ya afisa mkuu wa serikali ya kaunti ya Kilifi aliyekuwa akisimamia masuala ya uchumi wa baharini Rahab Karisa amekamatwa.

Diana Naliaka alikamatwa katika mpaka wa Kenya na Uganda mjini Busia na kufikishwa mahakamani.

Hakimu Mkuu wa mahakama ya Kilifi Justus Kituku aliwakubalia maafisa wa polisi kumzuilia Naliaka kwa siku 14 katika kituo cha polisi cha Kilifi huku uchunguzi ukiendelea.

Mfanyakazi huyo wa nyumbani wa marehemu Karisa anashukiwa kumuua kwa kumdunga kisu katika makazi yake eneo la Mnarani, kaunti ya Kilifi Alhamisi wiki iliyopita kabla ya kutoweka.

Rahab alikuwa tu amerejea kutoka ziara ya wiki moja nchini Italia wakati walizozana na shangazi yake na mhudumu huyo wa nyumbani.

Ripoti zinaashiria kwamba Rahab alikuwa anatafuta ukweli kuhusu kutoweka kwa shilingi elfu 32 kati ya shilingi laki moja ambazo alikuwa ameweka nyumbani.

Naliaka, mzaliwa wa kaunti ya Bungoma, alikamatwa akijaribu kuvuka mpaka kuingia nchini Uganda juzi Jumanne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here