Home Habari Kuu Mshukiwa wa kubadili kadi za simu akamatwa Thika

Mshukiwa wa kubadili kadi za simu akamatwa Thika

0

Mtu mmoja anayeshukiwa kuhusika katika udanganyifu wa kubadilisha kadi za simu amekamatwa mjini Thika. 

Emmanel Kiprono alikamatwa alipofika kwenye duka la kampuni ya Safaricom kubadilishiwa kadi ya simu akitumia kitambulisho bandia na cheti cha polisi alichodai alipatiwa katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi.

Idara ya upelelezi wa Jinai, DCI inasema aliposailiwa, Kiprono aliwaelekeza makachero katika nyumba moja iliyopo katika mtaa wa Zimmerman ambako simu ya mkononi inayotumiwa kusajili kadi za simu, vyeti vya polisi vilivyoghushiwa na vitambulisho vya kitaifa miongoni mwa vitui vingine vilipatikana. 

Mshukiwa mwingine kwa jina Everline Alulu Kimani aliwahi kukamatwa Septemba 19, 2023 na kushtakiwa kutokana na kisa kama hicho. 

“DCI inawashukuru wahudumu wa Safaricom ambao daima wako makini na huwaarifu polisi kuhusu washukiwa kama hao na inatoa wito kwa umma kuiga mfano huo ili kukomesha uhalifu,” ilisema idara ya upelelezi katika taarifa leo Alhamisi.  

Website | + posts