Mshukiwa mkuu wa sakata ya mafuta yenye thamani ya shilingi bilioni 7.6 amekamatwa.
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC inasema ilimkamata Yagnesh Devani leo Jumanne asubuhi akiwa kwenye ofisi zake jijini Nairobi.
Devani anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kupambana na ufisadi ili kujibu mashtaka dhidi yake.