Home Habari Kuu Uchunguzi: Mshukiwa mkuu wa mauaji ya Maigo yuko shwari kushtakiwa

Uchunguzi: Mshukiwa mkuu wa mauaji ya Maigo yuko shwari kushtakiwa

0
Mshukiwa wa mauaji ya Dkt. Erick Maigo.

Mwanamke ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji ya Kaimu Mhasibu Mkuu wa Nairobi Hospital Eric Maigo yuko katika hali shwari na akili razini kushtakiwa. 

Hii ni kulingana na uchunguzi uliofanywa na madaktari wa akili katika hospitali ya wagonjwa wa matatizo ya akili ya Mathari, kaunti ya Nairobi.

Kumekuwa na habari tatanishi kuhusu umri wake rasmi  baada ya mamake kusema alizaliwa mwaka 2003, kinyume cha taarifa za awali zilizosema mshukiwa alikuwa na umri wa miaka 18.

Mwanamke huyo wa kutoka mtaani Kibera alifikishwa mahakamani Septemba 27 mwaka huu, ambapo polisi walipewa muda wa majuma matatu kukamilisha uchunguzi kabla ya kufunguliwa mashtaka.

Mwili wa marehemu Maigo ulipatikana chumbani mwake katika mtaa wa Woodley, kaunti ya Nairobi Septemba 15 ukiwa na majeruha 25 ya kisu.

Website | + posts