Home Habari Kuu Mshukiwa mkuu katika mauaji ya Erick Maigo akamatwa

Mshukiwa mkuu katika mauaji ya Erick Maigo akamatwa

0
Mshukiwa wa mauaji ya Dkt. Erick Maigo.

Maafisa wa polisi wamemtia nguvuni mshukiwa mkuu katika mauaji ya Mkurugenzi wa Fedha wa Nairobi Hospital, Eric Maigo.

Kulingana na maafisa wa polisi wa makosa ya jinai, DCI, mshukiwa huyo wa umri wa miaka 16, alikamatwa katika eneo la Olympic mtaani Kibra jana Jumanne usiku.

Hii ni baada ya maafisa kupokea habari kutoka kwa wananchi juu ya aliko mshukiwa.

Kupitia mtandao wa Twitter, DCI ilisema mshukiwa huyo alipelekwa katika makao makuu ya DCI kuhojiwa kabla ya kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga.

Mwili wa Maigo ulipatikana nyumbani kwake Septemba 15 ukiwa na majeraha 25 ya kudungwa kisu.

“Tunawashukuru wananchi kwa kutoa habari kwa polisi zilizosaidia kukamatwa kwa mshukiwa huyo,” ilisema DCI.

Website | + posts