Home Habari Kuu Mshikilizi wa rekodi ya dunia Kelvin Kiptum afariki katika ajali

Mshikilizi wa rekodi ya dunia Kelvin Kiptum afariki katika ajali

0
2023 TCS London Marathon - Elite men race - Kelvin Kiptum (3). Winner of the men race.

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum alifariki dunia Jumapili usiku baada ya gari walimokuwa wakisafiria pamoja na kocha wake kuhusika katika ajali ya barabarani kwenye barabara ya Eldoret-Kaptagat.

Kiptum aliye na umri wa miaka 24 alikuwa ameandikisha rekodi mpya ya dunia katika marathon ya saa 2 na sekunde 35 mwezi Oktoba  mwaka jana wakati wa mbio za Chicago, rekodi iliyorasimishwa chini ya wiki mbili zilizopita.

Kulingana na kamanda wa polisi wa eneo la Kaptagat Peter Mulinge, Kiptum pamoja na kocha wake Gervais Hakizimana, walifariki papo hapo baada ya mwanariadha huyo kushindwa kulidhibiti gari lake na kugonga mti na kuingia ndani ya mtaro kwenye barabara ya Eldoret-Kaptagat.

Abiria wa tatu aliyekuwa kwenye gari hilo alipata majeraha na kukimbizwa hospitalini.

Rais wa shirikisho la Riadha Ulimwenguni Sébastien Coe ni miongoni mwa waliotoa risala za rambirambi kufuatia kifo hicho.

Kiptum pia alikuwa ameshinda mbio za London Marathon na pia alitawazwa mwanariadha bora wa mwaka katika mbio za masafa marefu mwaka uliopita.

Makiwa kwa familia ya marehemu Kelvin Kiptum.