Home Habari Kuu Msajili Mkuu wa Mahakama kuapishwa Jumatatu

Msajili Mkuu wa Mahakama kuapishwa Jumatatu

0

Msajili Mkuu wa Mahakama Winfridah Boyani Mokaya ataapishwa siku ya Jumatatu kuanzia saa nne asubuhi.

Mokaya ana tajriba ya uanasheria ya zaidi ya miaka 27.

Anarithi nafasi iliyoachwa wazi na Anne Amadi aliyeondoka miezi miwili iliyopita baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 10.

Uapisho wake umewekwa kwenye gazeti rasmi la seriakli na Jaji Mkuu Martha Koome siku chache baada ya Tume ya Huduma za Mahakama kufanya usaili na kumteua.

Mokaya atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano.

Aliwashinda wapinzani wengine sita waliokuwa wakiwania wadhifa huo kabla ya kutangaza kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.

Website | + posts