Home Kimataifa Msajili mkuu wa Mahakama asema sekta ya haki kwa watoto inahitaji ufadhili...

Msajili mkuu wa Mahakama asema sekta ya haki kwa watoto inahitaji ufadhili zaidi

0
kra

Msajili mkuu wa idara ya mahakama nchini Winfridah Mokaya amesema kwamba kuna haja ya kuongeza ufadhili wa mfumo wa kuhakikisha watoto wanapata haki nchini.

Hatua hiyo alisema itawezesha washikadau kupambana na vikwazo na changamoto zinazokumba watoto na kupiga jeki mipango ya utunzaji wa watoto na maslahi yao.

kra

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango makhsusi wa haki kwa watoto wa mwaka 2023 – 2028 wa baraza la kitaifa la utekelezaji wa haki nchini, Mokaya alisema utambuzi wa hitaji la ufadhili zaidi ni muhimu katika utekelezaji wa mpango uliozinduliwa.

“Tunaelewa kwamba bila ufadhili wa kutosha, azma yetu ya kuwa na vituo vinavyowafaa watoto, maafisa wa haki waliopatiwa mafunzo na ujuzi unaohitajika kushughulikia mahitaji ya watoto haitatimia.” alisema Mokaya.

Alitaja uzinduzi wa mpango huo makhsusi kuwa hatua kubwa, ishara ya matumaini na ushuhuda wa kujitolea kwa sekta ya haki kuhakikisha nyakati nzuri siku za usoni katika maisha ya kila mtoto nchini.

“Mpango tunaozindua ni ahadi yetu ya kubadilisha kabisa jinsi jamii na mfumo wa haki zinahusiana na watoto na kuwalinda.” aliongeza kusema msajili huyo mkuu wa idara yamahakama.

Aliwahimiza wadau wa sekta ya haki kwa watoto katika idara ya mahakama kuzingatia usemi wa aliyekuwa kiongozi wa Afrika Kusini Nelson Mandela kwamba moyo wa jamii unafunuliwa kupitia namna ambayo inawatunza watoto.

Mokaya aliahidi baraza la utekelezaji wa haki nchini NCAJ kwamba ataongoza juhudi za kuwaleta pamoja wadau wa sekta mbali mbali ili kushabikia, kulinda na kupiga jeki utekelezaji wa haki kwa watoto katika mifumo rasmi na isiyo rasmi.

Website | + posts