Home Burudani Msaidieni Annastacia Mukabwa jamani, Gloria Muliro awarai wafuasi

Msaidieni Annastacia Mukabwa jamani, Gloria Muliro awarai wafuasi

0
kra

Mwimbaji wa nyimbo za injili Gloria Muliro amewarai wafuasi wake na wengine kuchangia gharama za matibabu ya mwimbaji mwenza Annastacia Mukabwa.

Kwa mujibu wa bango alilochapisha katika ukurasa wake wa kitandazi, mwimbaji huyo wa nyimbo maarufu kama vile “Narudisha”, amedokeza kuwa Annastacia anastahili kusafiri hadi nchini India kupokea matibabu ya dharura.

kra

Ameomba yeyote kuchangia chochote alichonacho kugharimia matibabu ya Annastacia anayefahamika sana kutokana na wimbo wake wa “Kiatu Kivue”.

Habari za kuugua kwa mwimbaji huyo tajika ambaye wengi wamedhani anatokea nchi jirani ya Tanzania ingawa yeye ni Mkenya zimewashtua mno wafuasi wake huku wengi wakitaka maelezo zaidi kuhusu hali yake.

Kwenye mtandao, watu wengi wamemmiminia sifa kochokocho kutokana na nyimbo zake za injili zinazozidi kuwabariki na kumtakia nafuu ya haraka.

Hii si mara ya kwanza kwa Annastacia kukumbwa na hali ngumu kwani miaka kadhaa iliyopita, alikutana na Mama wa Taifa Rachel Ruto na kumwelezea shida yake.

Wiki chache baadaye, alialikwa nyumbani kwa Rachel huko Sugoi kwa mkutano wa injili wa wiki moja.

Baadhi ya nyimbo zake zingine maarufu ni Kalenda ya Mungu, Manamba na Watangoja Sana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here