Home Habari Kuu Mradi wa maji ya Ziwa Victoria wazinduliwa Singida Tanzania

Mradi wa maji ya Ziwa Victoria wazinduliwa Singida Tanzania

0
kra

Rais wa nchi jirani Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua mradi mkubwa wa maji ya kutoka Ziwa Victoria hadi eneo la Shelui Mkoani Singida leo Oktoba 17, 2023.

Mradi huo uligharimu shilingi bilioni 24.47 pesa za Tanzania kwa awamu ya kwanza, fedha ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Exim nchini India.

kra

Awamu ya kwanza ya mradi huo ilikamilika Agosti 11, 2023 na utafaidi wakazi wapatao elfu 40 wa Vijiji vya Tinde-Shinyanga na Shelui-Singida ambao watapata huduma ya maji safi na salama.

Awamu ya pili ya mradi huo itagharimu shilingi bilioni 16.2 pesa za Tanzania.

Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Kahama (KASHWASA) ndiyo inasimamia ujenzi wa mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria.

Viongozi kadhaa walihudhuria uzinduzi wa mradi huo kama vile Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, Balozi wa India nchini Tanzania, Binaya Srikanta Pradhan, Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.