Home Burudani Mr Ibu asherehekea siku ya kuzaliwa hospitalini

Mr Ibu asherehekea siku ya kuzaliwa hospitalini

0

Mwigizaji wa filamu za Nollywood za Nigeria John Ikechukwu Okafor, maarufu kama Mr. Ibu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa katika chumba cha wagonjwa hospitalini.

Kwenye video iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya Instagram, Okafor ambaye anaonekana kuzidiwa na uchungu amezingirwa na watu wa familia yake ambao wanasikika wakimwimbia nyimbo huku akikata keki.

Haijabainika mzee huyo ambaye ametimiza umri wa miaka 62 anaugua nini lakini mguu wake mmoja unaonekana umefura na katikati ya vidole amepakwa dawa ya rangi nyeupe.

Wengi wa wafiasi wake kwenye mitandao wamemwandikia jumbe za heri njema wakiamini kwamba atapona. Haijulikani amekuwa hospitalini humo kwa muda gani.

Mwaka 2022 mzee huyo alilazwa hospitalini mara mbili, kwanza mwezi Machi ambapo baadaye alielezea kwamba alitiliwa sumu katika hafla moja ambayo alihudhuria mjini Abuja. Wakati huo alilazwa hospitalini kwa muda wa mwezi mmoja.

Mara ya pili alilazwa mwezi Mei tarehe 25 wakati yeye na mkewe walistahili kusherehekea miaka 12 ya ndoa. Mkewe kwa jina Stella ndiye alichapisha habari za Okafor kulazwa hospitalini bila kuelezea kilichokuwa kikimsibu.

Website | + posts