Home Burudani Mpishi Maliha aweka rekodi mpya ya kupika kwa saa 150

Mpishi Maliha aweka rekodi mpya ya kupika kwa saa 150

0
Chef Maliha Mohammed poses for a photo as she attempts to break the Guinness World Record for the longest individual cooking marathon

Mpishi maarufu wa Kenya, Maliha Mohammed ameandikisha rekodi ya dunia kwa kupika kwa muda mrefu zaidi akiwa pekee.

Maliha aiweka rekodi mpya duniani ya kupika kwa saa 150 na sekunde 11 akipika mfululizo kwa wiki moja.

Maliha amevunja rekodi ya awali ya saa 119 dakika 57 na sekunde 16 ya Mwingereza Alan Fisher iliyoandikishwa Novemba 7 mwaka huu.

Mpishi Maliha Mohammed akionyesha muda aliotumia kupika

Mpishi huyo awali mwezi Agosti mwaka huu alikuwa ameandikisha rekodi mpya ya dunia alipopika kwa saa 90 na dakika 15 akivunja rekodi iliyokuweko ya saa 68 dakika 30 na sekunde 1.

Maliha atasubiri rekodi yake kurasimishwa kwenye kitabu cha Guiness ndani ya siku tano zijazo.

Website | + posts