Home Kimataifa Mpango wa usaidizi wa kisheria wa Rais Samia kuendelea hadi ufikie wananchi...

Mpango wa usaidizi wa kisheria wa Rais Samia kuendelea hadi ufikie wananchi wote

0

Waziri wa Masuala ya Katiba na Sheria nchini Tanzania Balozi Pindi Chana amesema kwamba wizara yake imejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba wananchi wote wananufaika na mpango wa usaidizi wa kisheria wake Rais Samia Suluhu almaarufu “Mama Samia Legal Aid”.

Kampeni hiyo inalenga kutoa huduma za kisheria bila malipo hasa katika masuala kama vile migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi na utunzaji wa watoto.

Waziri Chana aliongoza uzinduzi wa kampeni hiyo katika uwanja wa stendi ya zamani katika mkoa wa Singida, Januari 10, 2024.

Alielezea kwamba mpango huo wa huduma za bure utaendelezwa kwenye halmashauri zote za mkoa wa Singida kuanzia leo hadi Januari 19, 2024.

Wakazi wa mkoa wa Singida na maeneo jirani wamehimizwa kutumia vyema fursa hiyo ili kuhakikisha wanapata huduma na ufahamu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria.

Mpango wa “Mama Samia Legal Aid” ulianzishwa mwezi Aprili, 2023 na kufikia sasa mikoa mitano ambayo ni Dodoma, Manyara, Shinyanga, Ruvuma na Simiyu.

Idadi ya watu ambao wamepokea huduma chini ya mpango huo kufikia sasa ni 362,488 ambapo wanaume ni 179,874 na wananwake 182,615.

Migogoro karibu 6,365 ya ardhi, ndoa, mirathi na matunzo ya watoto ilipokelewa na 488 ilitatuliwa wakati wa kampeni na mingine inaendelea kutatuliwa.

Website | + posts