Home Taifa Mpango wa kurejea kazini wa wafanyakazi wa viwanja vya ndege waafikiwa

Mpango wa kurejea kazini wa wafanyakazi wa viwanja vya ndege waafikiwa

0
kra

Wafanyakazi wa viwanja vya ndege waliokuwa wakigoma kuanzia usiku wa manane jana sasa wameafikia makubaliano ya kurejelea kazi na wawakilishi wa mashirika husika na serikali.

Hii ni baada ya mkutano ulioongozwa na waziri wa uchukuzi Davis Chirchir na kuhudhuriwa na wawakilishi wa wafanyakazi hao kupitia chama chao cha KAWU na wasimamizi wa mashirika ya serikali yanayosimamia usafiri wa ndege nchini.

kra

Waliafikiana kwamba malalamishi ya wafanyakazi hao ambayo yalipokelewa leo, yatathminiwe kwa muda wa siku 10 na baada ya hapo mkutano mwingine uandaliwe ili majibu yatolewe.

Kutakuwa na wawakilishi wawili wa kila kundi lililohusika na kwamba wafanyakazi hawataadhibiwa kwa vyovyote kwa kushiriki mgomo wa leo.

Kuhusu mgomo wa Agosti 12, 2024, mamlaka inayosimamia viwanja vya ndege nchini KAA imekubali kuondoa kesi iliyokuwa imewasilisha mahakamani dhidi ya chama cha KAWU.

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura alisema kwamba mpango wa kuipa kamouni ya Adani usimamizi wa uwanja wa ndege wa JKIA ulikuwa katika kiwango cha pendekezo na mkutano huo uliafiki kwamba hakuna mapatano yatatiwa saini na kampuni hiyo kutoka India pasi na kujulisha wanachama wa chama cha KAWU.

Serikali kwa upande mwingine inasema kwamba suala hilo liko mahakamani na itatumia mchakato huo kuhakikisha inatoa taarifa zote kuhusu uboreshaji wa uwanja huo wa ndege.

Mahakama kuu ilisimamisha mipango yoyote ya kuuza au kukodisha uwanja wa JKIA kwa kampuni ya Adani katika ombi lililowasilishwa na chama cha wanasheria nchini LSK na tume ya kitaifa ya haki za binadamu KHRC.

Website | + posts