Home Habari Kuu Mpango wa kuajiri watendakazi vibarua wasimamishwa Laikipia

Mpango wa kuajiri watendakazi vibarua wasimamishwa Laikipia

0

Serikali ya kaunti ya Laikipia imetangaza kufutiliwa mbali kwa mchakato wa kuajiri wafanyikazi vibarua wa kaunti hiyo, saa chache kabla ya kuanza.

Akizungumza na wanahabari gavana wa kaunti hiyo Joshua Irungu alisema kwamba hatua hiyo imechochewa na mazungumzo na viongozi wengine wa kaunti.

Anasema walikubaliana kusitisha shughuli hiyo ili kutoa nafasi kwa kubuniwa kwa sera mwafaka za kuongoza shughuli hiyo ili kudhibiti uajiri katika kaunti ya Laikipia.

Irungu alihimiza utulivu kati ya wakazi wa kaunti hiyo wanapoendelea kulainisha mpango huo ili kuhakikisha usawa na haki.

Awali moango huo ulikuwa umepangiwa kuanza leo Agosti 23, 2023.

Website | + posts