Home Kimataifa Mpango ulioboreshwa wa Linda Mama kurejeshwa, asema Katibu Muthoni

Mpango ulioboreshwa wa Linda Mama kurejeshwa, asema Katibu Muthoni

0
kra

Katibu katika Idara ya Afya ya Umma Mary Muthoni amesema serikali imekusudia kurejesha mpango wa Linda Mama. 

Amesema mpango huo utakuwa na mafao yaliyoboreshwa kwa kina mama wajawazito.

kra

Kulingana na Muthoni, Wakenya wamekuwa wakitoa wito wa mpango huo kurejeshwa, wito ambao serikali imeitikia.

Amesema kwa sasa, kuna zoezi linaloendelea la kushirikishwa kwa Wakenya ambao wanatakiwa kutoa mapendekezo zaidi ya namna ya kuuboresha mpango huo.

Serikali inasema mpango wa Linda Mama utakuwa moja ya nguzo ya Hazina ya Bima ya Afya ya Jamii, SHIF ambayo hasa itagharimia malipo ya kina mama wajawazito kwa kutengewa bajeti yake.

Chini ya mpango huo ulioboreshwa, mafao yataongezwa kiasi cha kina mama wajawazito kutohitajika kugharimia chochote bila kujali ikiwa wamejifungua kwa njia ya kawaida au kupitia upasuaji.

Tayari fedha zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo huku serikali ikitafuta fedha zaidi za kuufadhili.

Mpango wa Linda Mama ulianzishwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta mwezi Juni mwaka 2013 kwa lengo la kuondolea kina mama wajawazito mzigo wa kulipia huduma za kujifungua na matibabu kwa watoto wanaozaliwa.

Kina mama hao walihitajika tu kujisajili na kupatiwa kadi maalum na kisha kupokea huduma bila malipo.

Website | + posts