Home Vipindi Mpangilio wa ujenzi wa vibanda wasifiwa Busia

Mpangilio wa ujenzi wa vibanda wasifiwa Busia

0
kra

Wafanyabiashara mjini Busia wamesifia mpangilio wa ujenzi wa vibanda vya kisasa ambavyo wanasema vimebadilisha sura ya mji huo.

Awali, mji huo ulisheheni matope, maji taka mrundiko wa taka, lakini kwa sasa, wenyeji wanasema angalau wamepata mazingira safi ya kufanyia biashara zao.

kra

Baadhi ya wafanyabiashara  wanaojihusisha katika sekta ya uchukuzi wamesema kwamba kwa sasa, wamepata afisi zao za kazi.

Waziri wa Ardhi na Ustawishaji wa Miji katika kaunti hiyo Peter Odima amesema kuwa wanafanya kila juhudi kuboresha sura ya mji huo.

Aliyasema hayo wakati mwakilishi wadi ya Burumba Tony Onyango ameitaka serikali ya kaunti ya Busia kuimarisha miundombinu mjini Busia kama vile mitaro ya kupitisha maji taka, kituo cha magari na usafi ili kuvutia biashara.