Home Habari Kuu Moto wazuka katika Jengo la Old Mutual

Moto wazuka katika Jengo la Old Mutual

0

Moto ulizuka jana usiku juu ya jumba la Old Mutual lililoko katika mtaa wa Upper Hill muda mfupi baada ya maonyesho ya fataki za kukaribisha mwaka mpya 2024.

Picha zilizosambaa mitandaoni zilionyesha moto na moshi mkubwa vikitoka kwenye sehemu ya juu ya jumba hilo linalofahamika sana kwa maonyesho ya taa na fataki.

Wataalamu wa kuzima moto hata hivyo walichukua hatua za haraka na kufanikiwa kuuzima haraka na kuzuia uharibifu zaidi.

Hakuna mtu aliripotiwa kujeruhiwa kwenye kisa hicho cha jana usiku.

Inaaminika kwamba ulipuaji wa fataki ndio ulisababisha moto huo lakini polisi wameanzisha uchunguzi ili kubaini hilo na kuzuia visa kama hivyo siku za usoni.

Website | + posts