Home Kimataifa Moto wateketeza nyumba za makazi usiku huko Lang’ata

Moto wateketeza nyumba za makazi usiku huko Lang’ata

0
kra

Familia kadhaa zimeachwa bila makazi baada ya moto kuteketeza nyumba zao usiku wa kuamkia leo katika eneo la Southlands, Kijiji eneo bunge la Lang’ata katika kaunti ya Nairobi.

Kulingana na shirika la Msalaba Mwekundu, moto huo ulizuka yapata saa mbili usiku na kuzimwa kabisa kufikia saa nne na dakika 20.

kra

Hayo yalifanikishwa kwa ushirikiano kati ya wazima moto wa serikali ya kaunti ya Nairobi, wahudumu wa shirika la msalaba mwekundu na kundi la jamii ya eneo hilo la kushughulikia majanga.

Wakazi waliohojiwa na wanahabari walisema kwamba wazima moto wa serikali ya kaunti ya Nairobi walifika katika eneo la tukio saa moja baada ya moto kuzuka na kwamba gari zao za zima moto hazikuwa na maji na hivyo kupunguza kasi ya mpango wa kuzima moto huo.

Ukosefu wa barabara zinazotoshea magari hayo ya zimamoto pia ulichelewesha shughuli ya kuzima moto kwani wazima moto walilazimika kupitia Onyonka Estate ili kufikia eneo la tukio.

Kama hatua za mwanzo, wakazi wa maeneo ya karibu walishauriwa kutolaza watoto wachanga hadi moto huo uzimwe kabisa wasije wakavuta moshi.

Website | + posts