Home Michezo Morocco yatangaza kikosi kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia

Morocco yatangaza kikosi kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia

0

Kocha wa Morocco Walid Regragui ametaja kikosi cha Atlas Lions, kitakachoshiriki mechi mbili za mwezi ujao kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.

Morocco wameratibiwa kuchuana na Zambia na Congo mwezi ujao.

Kocha huyo amewaita kikosini kwa mara ya kwanza wachezaji Oussama Targhalline wa klabu ya Le Havre, na kipa wa klabu ya AS FAR El Mehdi Benabid .

Makipa walioitwa kikosini wanajumuisha Yassine Bounou, Munir El Kajoui na Benabid .

Mabeki ni Achraf Hakimi, Romain Saiss, Nayef Augerd, Noussair Mazraoui, Yahya Attiat Allah , Achraf Dari, Abdelkabir Abqar, Mohamed Chibi na Chadi Riad.

Viungo ni pamoja na Amir Richardson,Brahim Diaz, Oussama El Azzouzi ,Bilal El Khannouss, Azzedine Ounahi,Sofyan Amrabat, Oussama Targhaline, na Ismael Saibari.

Soufiane Rahimi, Amin Adli, Hakim Ziyech, Ayoub El Kaabi, Youssef En-Nesyrri, Ilias Ben Sghir na Ilias Akhomach.

Morocco itachuana na Zambia katika mechi ya kufuzu kwa ya kwanza kufuzu kwa kombe la Dunia dhidi ya Zambia Juni 7, mjini Agadir kabla ya kucheza mchuano wa kirafiki dhidi ya Congo siku nne baadaye.

Atlas Lions imo kundi E la kufuzu wa kombe la dunia mwaka 2026 pamoja na Zambia, Niger, Congo, Tanzania na Eritrea.

Kipute cha kombe la Dunia mwaka 2026 kitaandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Canada, Marekan na Mexico.