Home Michezo Morocco watwaa kombe la AFCON U23

Morocco watwaa kombe la AFCON U23

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Morocco kushinda kombe hilo huku wakiandaa fainali hizo kwa mara ya pili baada ya mwaka 2011.

0
kra

Wenyeji Morocco ndio mabingwa wa makala ya nne ya kipute cha kombe la mataifa ya Afrika kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 23, baada ya kutoka nyuma na kuwaangusha mabingwa watetezi Misri mabao 2-1 Jumamosi usiku ugani prince Moulay Abdellah jijini Rabat.

Mahmoud Sabre afungua ukurasa kwa Misri kunako dakika ya 9 na kisha kupigwa umeme kwa mchezo mbovu dhidi ya mshambulizi wa Morocco Abdessamad Ezzalzouli, dakika 8 baade.

kra

Yanis Begraoui alisawazisha kwa wenyeji katika dakika ya 37 na matokeo kusalia hivyo hadi dakika 90 na 15 za kipindi cha kwanza .


Oussamna Targhalline aliunganisha mkwaju wa adhabu wake Ezzalzouli na kuwanyanyua mashabiki wa nyumbani kwa bao la pili .

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Morocco kushinda kombe hilo huku wakiandaa fainali hizo kwa mara ya pili baada ya mwaka 2011.

Morocco,Misri na na Mali zilijikatia tiketi kushiriki mashindano ya Olimpiki mwaka ujao jijini Paris Ufaransa.