Limbukeni Morocco almaarufu Atlas Lioneses wameigutisha Colombia baada ya kuwacharaza bao moja kwa nunge katika mechi ya kundi H na kufuzu kwa raundi ya 16 bora ya Kombe la Dunia kwa vipusa kwa mara ya kwanza.
Anisa Lahmari alipachika bao pekee na ushindi kwa Morocco kunako dakika ya nne ya ziada katika kipindi cha kwanza, akijibu mkwaju wa penalti wa Chizlabe Chebbak uliokuwa umepanguliwa na kipa wa Colombia.
Morocco walimaliza katika nafasi ya pili kundi H kwa pointi 6 sawia na viongozi Colombia.
Morocco wanajiunga na mabingwa wa Afrika, Afrika Kusini, na Nigeria katika raundi ya 16 bora.
Atlas Lionesses watamenyana na Ufaransa katika mchuano wa mwisho wa raundi ya 16 bora.