Home Kimataifa Morocco na Israel zatia saini mkataba wa ushirikiano katika kilimo

Morocco na Israel zatia saini mkataba wa ushirikiano katika kilimo

Mkataba huo utasababisha kuzinduliwa kwa kituo cha pamoja cha miradi ya teknolojia ya kilimo na maji.

0
Mawaziri wa Kilimo wa Morocco na Israel, pamoja na jumbe zao.

Waziri wa kilimo wa Morocco Mohamed Sadiki ametia saini mkataba wa ushirikiano na mwenzake wa Israel siku ya Alhamisi, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kwenye masuala ya kilimo na maji kati ya mataifa hayo mawili.

Mkataba huo sasa unafungua njia ya ushirikiano wa timu kutoka mataifa hayo mawili, kufanya kazi pamoja wakati kukiwa na mpango wa kuzindua kituo cha masomo ya kilimo.

Pia mkataba huo utasababisha kuzinduliwa kwa kituo cha pamoja cha miradi ya teknolojia ya kilimo na maji.

Mkataba huo umefanyika wakati wa kongamano la pili la Afya barani Afrika likiandaliwa, likilenga kupunguza hatari za kiafya na ambalo limehudhuriwa na Israel mjini Marrakesh.

Aidha ushirikiano huo pia utawezesha mataifa hayo kubadilishana ujuzi wa kukabiliana na changamoto zinazokumba mataifa hayo mawili katika sekta ya kilimo.

Website | + posts
VOA
+ posts