Home Michezo Morans yafuzu robo fainali ya FIBA Afrocan

Morans yafuzu robo fainali ya FIBA Afrocan

Morans ilishindwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwenye fainali ya makala ya mwisho mwaka 2019.

0
Timu ya taifa ya wanaume ya mpira wa vikapu Kenya Morans. Picha/Hisani.

Timu ya taifa ya wanaume ya mpira wa vikapu Kenya Moran’s ilifuzu kwa robo fainali ya michuano inayoendelea ya FIBA Afrocan licha ya kushindwa alama 63-66 na Gabon kwenye mechi yake ya pili ya kundi A mjini Luanda, Angola.

Kenyan Morans ilikabiliwa na ukinzani mkali kwenye robo ya kwanza walionyakua alama 16-15. Morans ilishinda robo ya pili alama 16-12 na kulazimu mechi hiyo kwenda mapumzikoni Kenya ikiongoza alama 32-27.

Aidha, Gabon ilirejea kwa vishindo na kushinda robo ya tatu na nne alama 27-18 na 13-12 mtawalia na kuandikisha ushindi wa alama 66-63.

Kikosi hicho cha kocha Cliff Owuor kilimaliza katika nafasi ya kwanza Kundini A mbele ya Kodivaa na Gabon.

Kenya Morans ilishindwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye fainali ya makala ya mwisho mwaka 2019.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here