Home Michezo Moraa,Komen na Chebet wawika Doha

Moraa,Komen na Chebet wawika Doha

0
kiico

Bingwa mtetezi wa Dunia Mary Moraa, alianza vyema msimu alipotwaa ushindi wa mita 800 katika mkondo wa tatu wa Diamond League wa Ijumaa usiku mjini Doha,Qatar.

Moraa alistahimili ukinzani kutoka kwa mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mashinadno ya ukumbini Jemma Reekie na kushinda akitumia  muda wa dakika 1 na sekunde 57.91 .

Bingwa wa Dunia katika mbio za nyika Beatrice Chebet, alistahimili ushindani mkali kutoka kwa Ejgayehu Taye wa Ethiopia na kutwaa ushindi kwa dakika 14 sekunde 26.98.

Bingwa wa michezo ya Afrika Brian Komen, aliashiria ukakamavu wa hali ya juu akimshinda bingwa wa zamani wa dunia Timothy Cheruiyot katika mita 1500.

Komen aliziparakasa mbio hizo kwa dakika 3 sekunde 32.43, akifuatwa na Cheruiyot, huku Reynold Kipkorir akimaliza tatu.

Mshindi wa nishani ya shaba ya Abraham Kibiwott alimaza wa pili katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na Maji, huku Nelly Chepchirchir akiambulia nafasi ya tatu katika mita 1500 wanawake.

kiico