Home Kimataifa Moraa na Odira wajaa nusu fainali Chebet atapa Olimpiki ya...

Moraa na Odira wajaa nusu fainali Chebet atapa Olimpiki ya Paris

0
PARIS, FRANCE - AUGUST 02: Tsige Duguma of Team Ethiopia and Mary Moraa of Team Kenya compete during the Women's 800m Round 1 on day seven of the Olympic Games Paris 2024 at Stade de France on August 02, 2024 in Paris, France. (Photo by Steph Chambers/Getty Images)
kra

Bingwa wa Dunia wa mita  800 Mary Moraa na mshindi wa nishani ya fedha ya Afrika  Lillian Odira walijikatia tiketi kwa nusu fainali ya Olimpiki Ijumaa usiku jijini Paris, huku Vivian Chebet akikosa .

Chebet alikuwa wa kwanza kujitosa uwanjani katika mchujo wa tatu alipomaliza wa tano akiwa nje ya  nafasi tatu za moja kwa moja.

kra

Mwanariadha huyo atarejea Jumamosi kwa mchujo wa kuwanIa tiketi ya nusu fainali ya Jumapili hii, kabla ya fainali kuandaliwa Jumatatu.

Moraa aliziparakasa mbio hizo kwa dakika 1 sekunde 57.95,nyuma ya mshindi Tsige Duguma wa Ethiopia aliyesajili dakika  1:57.90.

Odira alifuzu kwa semi fainali aktumia kasi yake ya mwisho na kuchukua nafasi ya tatu kwa dakika 1 sekunde 58.88.

Awali Ijumaa jioni  timu ya Kenya ya mita 400 mseto kupokezana kijiti, ilikosa kufuzu kwa fainali baada ya kumaliza ya saba katika mchujo wa kwanza wa nusu fainali.

Timu ya Marekani ilivunja rekodi ya Dunia katika shindano hilo.

Website | + posts