Home Kimataifa Moraa atwaa dhahabu huku Jepng’etich akinyakua fedha Peru

Moraa atwaa dhahabu huku Jepng’etich akinyakua fedha Peru

0
kra

Sarah Moraa na Marion Jepng’etich waliishindia Kenya nishani za dhahabu na fedha mapema Jumamosi, katika makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 mjini Lima,Peru.

Moraa,ambaye pia ni bingwa wa Afrika aliongoza kutoka mwanzo hadi mwisho akitumia dakika 2 na nukta 36 kunyakua dhahabu ya pili ya Kenya katika mashindano hayo.

kra

“Nimefurahi sana kushinda dhahabu hii,ikiwa ni dhahabu yangu ya kwanza nikishiriki mashindano ya dunia kwa mara ya kwanza.Mimi hupenda kuongoza kutoka mwanzo ila leo sikutarajia kushinda dhahabu ila nafurahi nimeshinda dhahabu.”akasema Moraa

Marion Jepng’etich alishinda medali ya fedha katika fainali ya mita 3,000, akizikamilisha kwa dakika 8 sekunde 52.37,nyuma ya Aleshign Baweke wa Ethiopia aliyetwaa dhahabu huku shaba ikimwendea mwenzake Marta Alemayo .

Hata hivyo matumaini ya Wakenya kupata nishani katika fainali ya mita 800 wnaume yaliyeyuka baada ya Phanuel Kipkoesgei Koech na Kelvin Kimutai Koech kumaliza katika nafasi za 5 na 7 mtawalia.

Berhanu Ayansa wa Ethiopia alishinda dhahabu kwa muda wa dakika moja sekunde 46.86,wakati Peyton Craig wa Australia na Ko Ochiai wa Japan wakishinda fedha na shaba mtawalia.

Wakenya watarejea uwanjani katika siku ya mwisho Jumamosi usiku kuwania medali wakiongozwa na nahodha Edmund Serem, atakayeshiriki fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji akishirikaina na mwenzake mathew Kosgei.

Miriam Chemutai na Mary Nyaboke pia watashiriki fainali ya mita 1,500.

Kenya ni ya 6 kwenye msimamo kwa jumla ya medali 5 dhahabu 2 fedha 2 na shaba 1.

Marekani inaongoza kwa dhahabu 4 fedha 4 na shaba 4, baada ya kuikwatua Ethiopia hadi nafasi ya pili kwa dhahabu 4 fedha 2 na shaba moja ,wakati China ikiwa ya tatu kwa dhahahbu 3 fedha 3 na shaba 3.

Website | + posts