Home Habari Kuu Mombasa kupata hospitali moja ya level 6, asema Ruto

Mombasa kupata hospitali moja ya level 6, asema Ruto

0

Rais William Ruto amesema atashirikiana na wabunge ili kuipandisha hadhi ya hospitali ya Mombasa hadi kiwango cha level 6.

Akizungmza Jumapili katika eneo la Mama Ngina Water Front kaunti ya Mombasa, Rais Ruto amesema serikali itahitaji kati ya shilingi bilioni 5 hadi 10, ili kupandisha hadhi na kuifanya kaunti hiyo kuwa na angalau hospitali moja ya kiwango cha level 6.

Ruto amesema haya huku akikariri kujitolea kwa serikali kutekeleza kikamilifu afya ya jamii kupitia kwa  wahamasishaji wa afya  nchini, ambao watakuwa wakipokea malipo ya kijikimu kila mwezi.

Website | + posts