Home Kimataifa Mokaya Frida Boyani ateuliwa Msajili Mkuu wa Mahakama

Mokaya Frida Boyani ateuliwa Msajili Mkuu wa Mahakama

Mokaya sasa anachukua wadhifa ulioachwa wazi na Ann Amadi ambaye alistaafu, na atahudumu kwa muhula wa miaka tano.

0
kra

Tume ya huduma za Mahakama JSC, imemteua Mokaya Frida Boyani kuwa msajili Mkuu wa idara ya Mahakama.

Mokaya sasa anachukua wadhifa ulioachwa wazi na Ann Amadi ambaye alistaafu, na atahudumu kwa muhula wa miaka tano.

kra

Akithibitisha uteuzi huo kupitia kwa taarifa leo Jumanne, Jaji Mkuu Martha Koome alimpongeza Mokaya huku akiwashukuru watu wengine sita waliochaguliwa kuwania wadhifa huo.

Mokaya ambaye ana tajiriba ya miaka 27 katika tasnia ya uana sheria, pia atahudumu kama Katibu wa tume ya huduma za Mahakama JSC.

Kabla ya uteuzi wake, Mokaya alihudumu wadhifa wa msajili wa idara ya Mahakama kuanzia mwaka 2012.

Alijiunga na idara ya Mahakama mwaka 1997 na amehudumu kama hakimu mkaazi, hakimu mkuu mkaazi, hakimu mwandamizi na hakimu mkuu mwandamizi.

Wengine waliosailiwa na tume ya JSC kwa wadhifa huo ni pamoja na Macharia Rose Wachuka, Ouma jack Busalile, Wambeti Ann Ireri, Ndemo Paul Maina, Kendagor Caroline Jepyegen na Kandet Kennedy Lenkamai.