Home Habari Kuu Mokaya aapishwa kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama

Mokaya aapishwa kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama

0

Winfridah Boyani Mokaya ameapishwa kuwa Msajili Mkuu mpya wa Mahakama. 

Mokaya alikula kiapo cha kuhudumu katika wadhifa huo wakati wa hafla iliyoongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome leo Jumatatu asubuhi.

Anarithi nafasi iliyoachwa wazi na Anne Amadi aliyeondoka miezi miwili iliyopita baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 10.

Aidha, yeye ni Msajili Mkuu wa Mahakama wa tatu kuwahi kuhudumu katika wadhifa huo baada ya Amadi na Mwakilishi wa Wanawake wa sasa wa kaunti ya Uasin Gishu Gladys Boss Shollei.

Mokaya ana tajriba ya uanasheria ya zaidi ya miaka 27 na atahudumu kwa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na anaweza akaongezewa miaka mingine mitano ya kuhudumu.

Aliwashinda wapinzani wengine sita waliokuwa wakiwania wadhifa huo kabla ya kutangazwa kuwa Msajili Mkuu mpya wa Mahakama.

Website | + posts