Home Michezo Mnyama Simba atinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya...

Mnyama Simba atinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya nne

0

Klabu ya Simba ya Tanzania ilijikatia tiketi kwa kwota fainali ya kombe la Ligi ya Mabingwa kwa mara ya nne baada ya kuikwatua Jwaneng Galaxy kutoka Botswana magoli sita bila jibu.

Mechi hiyo ya kuhitimisha ratiba ya kundi B ilisakatwa katika uchanjaa wa Benjamin Mkappa siku ya Jumamosi.

Ushindi huo ulihakikisha Simba wanamaliza katika nafasi ya pili kwa pointi 9 nyuma ya Asec Mimosas ya Ivory Coast huku Wydad Casalablanca ya Morocco waliomaliza kwa alama sawa 9 wakikosa kufuzu kwa robo fainali.

Tanzania itakuwakilishwa na timu za Yanga na Simba katika robo fainali.

Website | + posts